Duration 2:37

Makamu wa rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif amefariki, Sharif amefariki akiwa na umri wa miaka 77

34 135 watched
0
56
Published 17 Feb 2021

Makamu wa rais wa zanzibar, maalim seif sharif hamad amefariki. maalim seif sharif hamad amefariki hii leo akipokea matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili jijini Dar es Salaam. Rais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, amethibitisha kifo hicho na kutangaza siku saba za maombolezo. Kupitia mtandao wa ikulu ya zanzibar, rais dkt. hussein mwinyi amesema zanzibar na tanzania imempoteza kiongozi shupavu. lakini taarifa ya rais mwinyi haijaeleza iwapo kifo cha makamu wake kimetokana na maambukizi ya virusi vya korona ingawa taarifa za chama chake za awali mwezi huu ziliarifu kuwa maalim seif sharif aliambukizwa virusi vya korona na kulazwa kwa matibabu chini ya jopo maalumu la madaktari.. sharif amefariki akiwa na umri wa miaka 77

Category

Show more

Comments - 13