Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amewaomba wananchi kutomuingilia muekezaji wa eneo la shule ya msingi Mringa Kata ya Olorien ambaye anamiliki kihalali.
Murro alifika eneo hilo kupatanisha mgogoro wa wananchi ambao walikuwa wanalazimisha muwekezaji kuondoka eneo hili hivyo ikapelekea kuingilia kati na kuwataka wananchi kuwa wapole kwa kuwa pia serikali inapata kodi kutokana na eneo hilo