Duration 1:7

Wanawake watakiwa kuwa tayari kuwania nafasi za uongozi

225 watched
0
3
Published 20 Sep 2021

Katibu Tawala Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki amewahimiza wanawake kupendana wakati fursa za uongozi zinapotokea ili wawe na sauti ya pamoja ya kuingia katika nafasi mbali mbali za za kuiongoza jamii. Katibu Miza amesema hayo uwanja wa mustani ya Mkoani kwenye mkutano wa uzinduzi wa kamati ya uhamasishaji wanawake kuweza kudai haki zao za uongozi, ulioandaliwa na jumuiya ya PEGAO kupitia mradi wa ushirikishaji wanawake katika uongozi unaotekelezwa kwa masirikiano na jumuiya ya PEGAO,ZAFELA na TAMWA chini ya ufadhili wa ubalozi wa Norway. Amesema kile kitendo cha kwamba mwanamke hawezi kuongoza kimepitiwa na wakati na kwamba kinachohitajika kwao ni kujiamini na kujitayarisha kielimu ili wawe na uwezo mkubwa wa utowaji wa maamuzi. Kwa upande wake mratibu wa mradi huo Dina Juma amewataka wanawake kuitumia fursa iliyowekwa na serikali ili kuongeza idadi ya viongozi katika ngazi za maamuzi ili kufikia malengo ya meleniam ya kuwa na usawa wa kijinsi katika nyanja tofauti. Mapema Mkurugenzi wa jumuiya ya PEGAO Hafidh Abdi Said ametoa rai kwa jamii kuwachagua wanawake katika nafasi za uongozi kwani wanasifa ya kuongoza na waaminifu katika kazi zao. #UGATvFurafaYako

Category

Show more

Comments - 0